Hadithi ya Diploma ya Bitcoin
Hakuna kitu chenye nguvu kuliko wazo ambalo wakati wake umefika.
Hadithi hii inaanza El Salvador mwaka 2022, tulipoanzisha Diploma ya kwanza ya Bitcoin duniani ndani ya mfumo wa shule za umma. Hatukuomba ruhusa kwa serikali. Shule ilitualika, na wanafunzi 38 walihitimu mwezi Juni huo.
Baadhi walitukosoa kwa kupita njia rasmi. Wanafunzi wa kwanza walipovuka jukwaa, tulitangaza upanuzi kwenda shule ya pili siku iliyofuata.
Mwaka mmoja baadaye, serikali hiyo hiyo iliomba msaada kuanzisha elimu ya bitcoin. Ili kulinda uhuru wetu, tulikataa malipo na badala yake tukawafundisha mamia ya walimu wa shule za umma ili waendeshe programu wenyewe.
Mwezi Septemba 2022 tulifanya mtaala mzima kuwa wazi kwa umma (open source). Kile kilichoanza kama jaribio la ndani kikawa haraka harakati ya kimataifa.
Leo hii mtaala unasasishwa mara mbili kwa mwaka na kubadilishwa na walimu duniani kote.
Sasa unajumuisha utangulizi wa saa moja na programu kwa watoto wadogo.
Machi 2023 tulizindua Mtandao wa Elimu, jumuiya ya kimataifa inayojengwa juu ya misingi ya pamoja: uhuru, kutokuwa na upendeleo, kuongozwa na jamii, bitcoin pekee, elimu bora. Tangu wakati huo, walimu wametafsiri mtaala na kuupeleka katika nchi 41 kwenye mabara sita.
Kwa sababu kazi hii ni wazi kwa umma (open source), wengine wengi wanafundisha kwa uhuru bila sisi kujua au kutoa ruhusa.
Diploma ya Bitcoin inafanikiwa kwa sababu inaakisi kile inachofundisha: kuwezeshwa kupitia ubunifu usiohitaji ruhusa. Inakua kupitia ushirikiano, si ushindani. Kupitia athari, si faida.
Elimu ya bitcoin inayoongozwa na jamii kwa uhuru itabadilisha dunia. Tayari imeanza.
Kwa ajili ya dunia bora,
Timu ya My First Bitcoin, 2026